Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon apongeza wacomoro kwa uchaguzi wenye amani

Ban Ki-moon apongeza wacomoro kwa uchaguzi wenye amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza raia wa visiwa vya Comoro kwa kutimiza majukumu yao ya kisiasa na kushirikiana kwenye awamu ya pili ya uchaguzi wa rais iliyofanyika jumapili iliyopita.

Taarifa ya msemaji wake imetolewa baada ya Tume huru ya Kitaifa ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya awali ijumaa hii.

Bwana Ban amenukuliwa akisema ni hatua muhimu katika kudumisha demokrasia Comoros.

Aidha Katibu Mkuu amewasihi wadau wote wa kisiasa kutatua sintofahamu zao zitokanazo na mchakato wa uchaguzi kupitia njia halali.

Hatimaye amekariri msimamo wa umoja wa Mataifa, kwa ushirikiano na Muungano wa Afrika na wadau wengine, kuunga mkono jitihada za raia wa visiwa wa Comoro katika kukuza demokrasia, amani na utawala wa sheria kwa manufaa ya umma.