Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumbukizi ya mauaji ya kimbari ya Rwanda

Kumbukizi ya mauaji ya kimbari ya Rwanda

Miaka 22 iliyopita, kuanzia tarehe 7 mwezi Aprili, 1994 kwa siku 100, Rwanda ulishuhudiwa wakati mgumu zaidi katika historia yake.

Zaidi ya watu 800,000, hasa Watutsi, lakini pia Wahutu na Watwa wenye msimamo wa wastani waliuawa katika mauaji hayo ya kimbari.

Kwa mujibu wa Rais wa Baraza Kuu, mauaji hayo yamekuwa na madhara makubwa kwa raia wa Rwanda na ukanda mzima, hasa kwa sababu jamii ya kimataifa ilimeshindwa kutambua mapema dalili za mauaji hayo na kuchukua hatua zilizohitajika ili kuyazuia.

Kumbikizi ya mauaji ya kimbari ya Rwanda ambayo inafanyika kila mwaka kwenye ofisi mbali mbali za Umoja wa Mataifa, lakini pia katika jamii za wanayarwanda, ni njia ya kuwaenzi wahanga waliopoteza maisha yao, kusaidia manusura kusonga mbele na kujenga maridhiano.

Tuungane na Priscilla Lecomte ambaye amehudhuria hafla ya kumbukizi iliyofanyika wiki hii mjini New York Marekani