Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tetemeko kubwa laukumba mji wa Kumamoto Japan:OCHA

Tetemeko kubwa laukumba mji wa Kumamoto Japan:OCHA

Tetemeko la ukubwa wa 0.7 vipimo vya richter limekumba mji wa Kumamoto hii leo huko Kusini Magharibi mwa Japan. Hili ni tetemeko la pili baada ya lile la jana April 14 lililokuwa na ukubwa wa vipimo vya 6.5.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA tetemeko la jana limekatili maisha ya watu 9 na kujeruhi wengine zaidi ya 1000.

Pia limesema watu 7600 wamearifiwa kunda kwenye makazi ya muda huku umeme ukirejea karibu maeneo mengi yaliyoathirika.

Hata hivyo shirika hilo limesema bado nyumba 32,000 maji ya bomba hayajarejea.

Kwa mujibu wa Malaya ya Japani ya nyuklia hakuna uharibifu wowote kwenye mitambo na vinu vya nyuklia vilivyoarifiwa, pia tahadhari iliyowekwa awali kuhusu tsunami sasa imeondolewa.

Taarifa zaidi za athari za tetemeko la leo bado hajizapatikana na Umoja wa Mataifa unaendelea kufuatilia kwa karibu hali hiyo.