Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame unaendelea kuyaghubika maeneo ya Puntland na Somaliland

Ukame unaendelea kuyaghubika maeneo ya Puntland na Somaliland

Hali ya ukame mkali imeendelea kushika kasi katika majimbo ya Somaliland na Puntland.

Kwa mujibu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, watu milioni 1.7 wanahitaji msaada wa kibinadamu na wa kujikimu kimaisha.

Na watu 385,000 kati ya hao wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula huku wengine zaidi ya milioni moja wako katika hatari ya kutumbukia katika hali hiyo endapo hawatapata msaada.

OCHA inasema watoto pia wameathirika vibaya na hali hiyo ambapo karibu laki moja wenye umri wa chini ya miaka mitano wanakabiliwa na utapia mlo na wanahitaji matibabu haraka.

Shirika hilo limeongeza kwamba hadi sasa mahitaji yanavuka uwezo wa rasilimali zilizopo na limetoa wito wa msaada wa dola milioni 105 ili kuwafikia watu zaidi ya milioni Puntland na Somaliland.