Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera dhidi ya dawa za kulevya zimeangamiza wengi kuliko dawa zenyewe: Kazatchkine

Sera dhidi ya dawa za kulevya zimeangamiza wengi kuliko dawa zenyewe: Kazatchkine

Namna jamii inavyoshughulika tatizo la dawa za kulevya ni shida kuliko uwepo wa dawa zenyewe amesema mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya HIV/AIDS kwa ukanda wa Mashariki mwa Ulaya na Asia ya Kati Profesa Michel Kazatchkine.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York, Profesa Kazatchkine amesema dawa za kulevya yameangamiza watu wengi lakini sera za nchi zimeathiri watu zaidi.

Akizungumzia madhara ya kiafya yatokanayo na sera za kudhibiti dawa za kulevya, amesema zimeongeza machafuko ambayo kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, ni janga la kiafya akiangazia mfano wa Colombia na Mexico. Ya pili ni..

(SAUTI KAZATCHKINE)

‘‘ Ukimwi, na ugonjwa wa homa ya ini aina ya C. Inakadiriwa kuwa takribani watu milioni mbili wanaojidunga dawa wanaishi na HIV. Kwa upande wa homa ya ini aina C, idadi ni theluthi mbili ya wagonjwa. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Ulaya Mashariki, Asia Kati na Mashariki.’’

Madhara mengine amesema ni ugonjwa wa kifua kikuu, matumizi na ukosefu wa dawa kwa waathirika wa dawa za kulevya.