Skip to main content

FAO yapanua wigo kutafiti ugonjwa wa ukungu kwenye ngano

FAO yapanua wigo kutafiti ugonjwa wa ukungu kwenye ngano

Kuendelea kuenea kwa ugonjwa unaoshambulia ngano huko Asia ya Kati na Mashariki ya Kati kumetia hofu shirika la chakula na kilimo duniani, FAO na hivyo kuhaha pamoja na wadau wake kudhibiti ugonjwa huo.

FAO inasema ugonjwa huo unaosababisha ukungu kwenye mmea wa ngano ambao ni zao tegemewa katika kanda hizo pamoja, unatishia mavuno.

Kwa sasa FAO inapanua wigo wa ushirikiano na wadau ikiwemo kituo cha kimataifa cha utafiti wa kilimo kwenye maeneo kame, ICARDA na chuo kikuu cha Aarhus.

Ushirikiano huo unalenga kuwezesha mafunzo na ufuatiliaji na udhibiti wa ugonjwa huo wa ukungu kwenye ngano.

FAO katika taarifa yake imesema pia wamepanga kufanya tafiti katika nchi husika ili kuelewa kwa kina jinsi ugonjwa huo unavyoenea.