Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia bila polio inanyemelea wakati kampeni ya chanjo ya kihistoria ikianza:WHO

Dunia bila polio inanyemelea wakati kampeni ya chanjo ya kihistoria ikianza:WHO

Wiki ijayo inaanza kampeni kubwa y a haraka ya kimataifa na ya kihistoria ya mipango chanjo dhidi ya polio limesema shirika la afya duniani WHO.

Kati ya tarehe 17 Aprili na 1 Mai, nchi 155 duniani kote zitaacha kutumia njanjo aina ya trivalent (tOPV) inayotolewa kwa njia yam atone ambayo inawalinda watoto dhidi ya aina zote tatu za virusi vya polio , na badala yake kuanza kutumia chanjo aina ya bivalent OPV (bOPV), ambayo inawalinda watu dhidi ya virusi aina mbili vilivyosalia , aina ya 1 na 3.

WHO inasema juhudi hizo zitatoa ulinzi kamilifu kwa watoto dhidi ya polio hususani wale walio katika hatari ya kupata maambukizi. Hatua hii ya kuhamia kwenye chanjo nyingine kimataifa inafahamika kama “switch” na inawezekana kwa sababu virusi vya polio aina ya 2 vimeshatokomezwa .

Hatua hii imependekezwa na kundi la wataalamu linalohusika na mkakati na ushauri kuhusu chanjo na imeidhinishwa na baraza kuu la afya kama mkakati mzuri wa kutokomeza kabisa polio na kuwa na dunia huru bila virusi hivyo.