UNRWA yasononeshwa kuendelea kwa machafuko Yarmouk

UNRWA yasononeshwa kuendelea kwa machafuko Yarmouk

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina UNRWA, limeelezea kusikitishwa na madhila ya kibinadamu yanayowakumba raia kutokana na machafuko kati ya vikundi vyenye misisimo mikali huko Yarmouk.

Taarifa ya shirika hilo imesema kuwa tangu Aprili sita mapigano yamesababisha sio tu majeraha kwa raia lakini pia, athari za kisaikolojia, njaa na ukosefu wa maji safi na kuathiri takribani watu 6,000 katika eneno hilo.

UNRWA imetaka usitishwaji wa uhasama baina ya makundi kinzani, na kuheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu ili kuheshimu na kulinda maisha ya raia huko Yarmouk.

Hata hivyo shirika hilo limesema linafuatailia kwa karibu kwa mtizamo wa kurejesha ujumbe wa kibinadamu haraka iwezekanavyo ili kusaidia raia katika eneo hilo.