Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafirishaji haramu wa binadamu ukomeshwe: Rybakov

Usafirishaji haramu wa binadamu ukomeshwe: Rybakov

Tukio maalum la mjadala kuhusu kupinga usafirishaji haramu wa binadamu na utumikishwaji limefanyika hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo wadau wamejadili namna ya kukabiliana na suala hilo.

Akichangia mada katika mjadala huo ulioratibiwa na Belarus msaidizi wa Rais wa nchi hiyo katika masuala ya sera ya nje, Valentine Rybakov amesema hatau zaidi zainapaswa kuchukuliwa kukomesha baishara haramu ya usafirishaji wa binadamu ambayo ni inashika nafasi ya tatu katika orodha ya uhalifu wenye faida kubwa ya kifedha.

(SAUTI VALENTINE)

‘‘Agenda mpya ya maendeleo endelevu iliyopitishwa na viongozi wa dunia mwesi Septemba mwaka jana, inatoa maelezo bayana ya uimara wa nia yetu ya kukomesha uhalifu huu, sio kwa maneno tu lakini katika vitendo halisi.’’

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2014 ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na madawa ya kulevya na uhalifu UNODC, utumikishwaji kazini ni asilimia 40 ya uhalifu.