Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusake mbinu kudhibiti matumizi mabaya ya intaneti- Ban

Tusake mbinu kudhibiti matumizi mabaya ya intaneti- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka tathmini ya miaka kumi ya mkakati wa kukabiliana na ugaidi iibue maridhiano baina ya nchi wanachama kwa lengo la kujenga umoja wakati huu ambapo magaidi wanasaka kuleta mgawanyiko.

Ban amesema hayo akihutubia Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wakati wa mjadala kuhusu harakati za kukabiliana na ugaidi ulimwenguni wakati huu ambapo magaidi wanahaha kusajili watu kwenye vikundi vyao kupitia njia mbali mbali ikiwemo mitandao ya kijamii, hivyo akasema..

(Sauti ya Ban)

“Lazima tudhibiti matumizi mabaya ya intaneti na mitanadao ya kijamii kwenye kujengea misimamo mikali vijana na kuwaingiza kwenye vikundi hivyo. Tusake suluhu ya kimataifa ikihusisha taasisi za kikanda, serikali, sekta binafsi na mashirika ya kiraia. Mikakati hii itahitaji sheria na uzingatiaji katika ngazi ya taifa."

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa zaidi ya watu Elfu Thelathini kutoka maeneo mbali mbali duniani wamejiunga na kampeni za Da’esh’s  au ISIS huko Iraq na Syria na kuwa tishio la usalama kwa nchi zao au nchi nyinginezo pindi wanaporejea.