Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inatoa muongozo mpya wa kutibu homa ya ini aina C

WHO inatoa muongozo mpya wa kutibu homa ya ini aina C

Katika mtazamo wa kuendelea na mchakato wa kusaka tiba mpya ya homa ya ini aina C shirika la afya duniani WHO linatoa muongozo mpya wa matibabu.

Muongozo huo unachagiza kuingia katika dawa mpya ambayo inafanya kazi vizuri zaidi na inauwezekano wa kutibu watu wengi wanaoishi na maambukizi ya homa ya aini aina C.

WHO ilitoa mapendekezo yake ya kwanza kabisa kuhusu tiba ya homa ya ini aina C mwaka 2014 na tangu wakati huo dawa nyingi mpya zimetolewa na kuuzwa.

Inakadiriwa kuwa watu milioni 130 hadi milioni 150 wameathirika na homa ya ini aina C na kila mwaka inakadiriwa watu laki 7 hufa kwa athari zitokanazo na ugonjwa huo ikiwemo kuvimba kwa ini, saratani ya ini na ini kushindwa kufanya kazi.