Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake na wasichana bado hatarini Nigeria, tangu utekaji wa Chibok

Wanawake na wasichana bado hatarini Nigeria, tangu utekaji wa Chibok

Mashirika ya kibinadamu nchini Nigeria yamesema kuwa idadi kubwa ya wanawanake na wasichana Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo bado wanakumbwa na hatari kubwa, wakati hatma ya wasichana 219 wa shule ya Chibok waliotekwa nyara miaka miwili iliopita ikiwa bado haijulikani. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Mratibu wa kibinadamu nchini Nigeria, Fatma Samoura, amesema wakiwa mikononi mwa Boko Haram, wasichana wa Chibok na wengine wengi wameteseka kwa kulazimishwa kuingia katika kikundi hicho cha kigaidi, ndoa za lazima, utumwa wa kingono na ubakaji, huku wakitumiwa pia kubeba mabomu.

Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini Nigeria, Jean Gou, amesema wanawake na wasichana kati ya 2,000 na 7,000 wametekwa, wakiishi katika utumwa wa kingono.

Akizungumza kuhusu hali hiyo, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu watoto katika vita, Leila Zerrougui, amesema..

(Sauti ya Leila)

“Tukumbuke kwamba hii ndiyo hatma ya watoto wa Nigeria, iliyokuwepo hata kabla. Kilichofanyika kwa wasichana wa Chibok kilikuwa tu tukio lililouwezesha ulimwengu kujua kinachofanyika Nigeria.”