Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Canada yatoa dola milioni 40 kusaidia vita dhidi ya polio Pakistan

Canada yatoa dola milioni 40 kusaidia vita dhidi ya polio Pakistan

Serikali ya Canada imetangaza kuwa itatoa mchango wa dola milioni 40 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, kusaidia nchi ya Pakistan katika juhudi zake za kutokomeza ugonjwa wa polio, ambao husababisha kupooza viungo vya mwili.

Mchango huo wa Canada utaimarisha usaidizi kwa jamii mashinani zinapokabiliana na polio, katika uhamasishaji, na katika kusaidia mradi wa usajili na mafunzo kwa watoaji chanjo kwa jamii mashinani, ambao unatekelezwa na Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF).

Kupitia mchango huo wa fedha, Shirika la Afya Duniani (WHO), litaimarisha operesheni za utoaji chanjo ya ziada, kampeni za chanjo na ufuatiliaji wa juhudi za kugundua virusi vya polio.