Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hawa Bangura ziarani Mali

Hawa Bangura ziarani Mali

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono vitani, Zainab Hawa Bangura, ameanza ziara ya siku tano nchini Mali.

Lengo la ziara yake ni kuangazia juhudi za kupambana na unyanyasaji wa kingono kwa mujibu wa makubaliano ya amani ya Algiers, wakati huu ambapo ukatili huo unatumiwa  kama silaha ya vita.

Bi Bangura amekutana na Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini Mali DAVIDSE KOEN na Waziri wa Wanawake, Watoto na Familia nchini humo OUMOU SANGARE BA.

Atakutana pia na wawakilishi wengine wa mamlaka za serikali ya Mali.