Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaendelea Jamhuri ya Congo: Zeid

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaendelea Jamhuri ya Congo: Zeid

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein amesema kumekuwa na ripoti za kutisha za ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Jamhuri ya Congo unaosababishwa na operesheni za usalama za serikali katika eneo la pool kusini mwa mji mkuu Brazzaville . John Kibego na ripoti kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Zeid amesema tangu uchaguzi wa Rais wa Machi 20 kumekuwa na ripoti kwamba operesheni zimekuwa zikifanywa dhidi ya viongozi wa upinzani na wafuasi wao wanaodaiwa kushambulia kituo cha polisi katika eneo la kusini mwa mji mkuu mnamo April 4.

Serikali imetangaza kuuawa kwa watu 17 kufuatia operesheni hizo za usalama wakiwemo wanajeshi watatu na watu wengine wengi kujeruhiwa. Zeid ameongeza kuwa taarifa zingine zinasema idadi kubwa ya watu wamekamatwa, kuteswa kizuizini ,kuuawa na kutawanywa katika eneo la Pool.

Cecil Pouliy ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva.

(Sauti ya Cecil)

“Tunaitaka serikali ihakikishie wadau wa masuala ya kibinadamu wanapata fursa haraka kuingia eneo la Pool. Na vikosi vya serikali vizingatie sheria za kimataifa za kibinadamu kwenye operesheni zao za kijeshi”