Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yahofia maelfu ya watu waliokimbia machafuko-DRC

OCHA yahofia maelfu ya watu waliokimbia machafuko-DRC

Maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wameelezea wasiwasi wao kuhusu hatma ya watu 35,000 waliokimbia wiki tatu zilizopita kutoka maeneo ya Mpati, Wilaya ya Masisi Kivu ya Kaskazini kufuatia mapigano baina ya jeshi la DR Congo na makundi yenye silaha. Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Maafisa hao wamesema tangu Machi 27 maeneo matano yanayohifadhi wakimbizi wa ndani yamesalia tupu na kuwalazimisha maelfu ya watu kusaka hifadhi kwenye vijiji vya jirani, ingawa baadhi ya waliokimbia vita wameaanza kurejea japo hali bado ni tete.

Kwa mujibu wa Florence Marchal ni mratibu wa mawasiliano wa mashirika ya kibinadamu nchini DRC amesema siku chache zilizopita imekuwa vigumu sana kwa wakimbizi wa ndani kuondoka au kurejea kwenye kambi wakizuiwa na mapigano na watoa misaada wanakabiliwa na changamoto

(SAUTI YA FLORENCE)

“Ni vigumu kufikia kwenye eneo hilo kwa sababu ya mapigano. Lakini kuanzia Aprili 4, baadhi ya mashirika ya kibinadamu yameweza kufikia kule ili kutathmini mahitaji. OCHA, Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu inaongoza sasa hivi ujumbe kwenye eneo hilo hilo.”