Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watoto wanaoshiriki kujitoa muhanga imeongezeka:UNICEF

Idadi ya watoto wanaoshiriki kujitoa muhanga imeongezeka:UNICEF

Idadi ya watoto wanaoshiriki mashambulizi ya kujitoa muhanga nchini Nigeria, Chad na Niger imeongezeka sana mwaka jana kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. John Kibego na taarifa kamili

(TAARIFA YA KIBEGO)

UNICEF katika ripotio yake mpya iliyotolewa leo imesema mwaka 2014 idadi ya watoto ilikuwa ni wanne na kuongezeka mwaka jana kufikia 44 na zaidi ya asilimia 75 ya watoto hao ni wasichana. Manuel Fontaine mkurugenzi wa kanda ya Afrika Magharibi na Kati wa UNICEF amesema ifahamike dhahiri kwamba watoto ni waathirika katika hali hii na sio wahalifu waanzilishi.

(Sauti ya Fontaine)

"Watoto hawa lazima wazingatiwe kama wahanga na sio wahalifu, na wakati mwingine wanakuwa hawajui hata kama wanabeba mabomu, na mara nyingi hudanganywa, uelewa wao wa kujua madhara ya kile wanachokifanya  ni mdogo sana , na inasikitisha kwamba haya yote yanajenga hofu na tuhuma dhidi ya watoto"

Akiongeza kuwa kuwarubuni watoto na kuwalazimisha kutekeleza vitendo vya mauaji imekuwa ni moja ya uhalifu mbaya saana Nigeria na katika nchi jirani.

Ikiwa imetolewa miaka miwli baada ya kutekwa watoto zaidi ya 200 wa Chibok, ripoti hiyo “zaidi ya Chibok”imeweka wazi mwenendo huo wa kusikitisha katika nchi nne zilizoathirika na Boko Haram miaka miwili iliyopita. Watoto takriban milioni 1.3 wametawanywa na athari za Boko Haram huku shule 1800 zikifungwa.