Skip to main content

Idadi ya watu ni zaidi ya kupanga uzazi- Kenya #CPD49

Idadi ya watu ni zaidi ya kupanga uzazi- Kenya #CPD49

Mkutano wa kamisheni  ya idadi ya watu na maendeleo ukiingia siku ya pili hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Kenya imesema inaungana na nchi zingine kuona jinsi ya kuimarisha takwimu kufanikisha maendeleo ya kiuchumi kwa kuzingatia ajenda ya maendeleo 2030.

Akihojiwa na idhaa hii, Mkurugenzi mkuu wa kamisheni ya Taifa ya idadi ya watu na maendeleo nchini humo Dkt. Josephine Kibaru-Mbae amesema hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa..

(Sauti ya Dkt. Josephine)

Amesisitiza kuwa idadi ya watu ni zaidi ya kupanga uzazi na hivyo ni vyema kuelimisha wananchi kwa sababu..

(Sauti ya Dkt. Josephine)

Mkutano huo unatarajiwa kumalizika tarehe 15 mwezi huu.