Skip to main content

Baiskeli yabadili maisha mkoani Mbeya Tanzania

Baiskeli yabadili maisha mkoani Mbeya Tanzania

Baiskeli, chombo mashuhuri sana na cha kale, hutumika katika shughuli mbali mbali duniani. Kwa kutegemea na sehemu gani ya dunia, baiskeli hutumika kama njia ya usafiri katika sehemu ambapo usafiri ni duni, ama njia ya kujipatia kipato, lakini vile vile kama  njia ya kufanya mazoezi.

Lakini siyo hayo tu, kwani baiskeli imekuwa mashuhuri katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea katika utunzaji wa mazingira, kwani haitegemei mafuta zaidi ya nishati itengenezwayo na yule anayenyonga baiskeli ili ipate mwendo.

Je, ni vipi Baiskeli inaleta manufaa kwa wakazi wa Kyela, mkoani Mbeya Tanzania?..Basi ungana na Alex Punte wa Radio Washirika KyelaFM anayetuhabarisha zaidi.