Ripoti yazinduliwa kuhusu ukuaji viwanda unaotunza mazingira Afrika

11 Aprili 2016

Leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kumezinduliwa ripoti ya uchumi wa Afrika kwa mwaka 2016.

Maudhui ya ripoti hiyo ni maendeleo ya viwanda yaliyo rafiki kwa mazingira. Akihutubia uzinduzi wa ripoti hiyo, Mshauri Maalum wa umoja wa Mataifa kuhusu Afrika, Maged Abdelaziz amesisitiza kwamba maendeleo ya viwanda ndio ufunguo kwa kuleta ukuaji endelevu wa uchumi barani Afrika utakaozalisha ajira kwa vijana.

Aidha amesema hii ni fursa kwa nchi za Afrika kuepukana na hatua ambazo nchi zilizoendela zimepitia katika maendeleo ya viwanda yanayochafua mazingira, na hivyo kuepusha na madhara yake.

(Sauti ya Abdelaziz)

“Ufungo wa maendeleo ya uchumi rafiki kwa mazingira barani Afrika ni uwekezaji. Uwekezaji kwenye miundombinu rafiki kwa mazingira, ikiwemo miundombinu endelevu ya miji, teknolojia na nishati endelevu, na uwekezaji kwenye ngazi zote za elimu, hasa sayansi na teknolojia.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter