Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

De Mistura na Waziri Muallem wajadili mustakhbali wa Syria

De Mistura na Waziri Muallem wajadili mustakhbali wa Syria

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Staffan de Mistura, amekutana na leo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Walid Muallem, kwa lengo la kujadili maandalizi ya mazungumzo ya amani Geneva, ambayo yamepangwa kuanza mnamo Aprili 13, 2016.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari baada ya mkutano huo, Bwana de Mistura amesema mazungumzo hayo ya Geneva ni muhimu sana, kwani yatamulika masuala ya mpito wa kisiasa, utawala, na kanuni za kikatiba.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa suala la kuwezesha ufikishaji wa usaidizi wa kibinadamu kwa maeneo yote yaliyozingirwa, pamoja na kwa Wasyria wote, limeibuka katika mazungumzo yake na Waziri Muallem.

Aidha, amesema kuwa wamejadili kuhusu umuhimu wa kulinda na kuunga mkono sitisho la uhasama, ambalo ingawa ni hafifu, linapaswa kuendelezwa, na vitendo vyovyote vya uhasama kudhibitiwa.