Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto ndio wanobeba mzigo mkubwa wa machafuko Yemen:Zerrougui:

Watoto ndio wanobeba mzigo mkubwa wa machafuko Yemen:Zerrougui:

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya watoto na vita vya silaha Bi Leila Zerrougui pamoja na Dr. Peter Salama mkurugenzi wa kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wamesema watoto nchini Yemen ndio wahanga wakubwa wa vita.

Wamesema hivyo usitishjaji mapigano ulioanza rasmi leo ni fursa nzuri kwa pande zote kuchukua hatua kuimarisha ulinzi kwa watoto hao.

Wamesema mwaka jana Umoja wa mataifa umethibitisha ongezeko kubwa la ukiukwaji dhidi ya watoto unaofanywa na pande zote za mgogoro nchini humo.

Kwa mujibu wa takwimu za karibuni watoto 900 wameuawa ikiwa ni ongezeko la asilimia 7 ikilinganishwa na mwaka 2014.Idadi ya watoto wanaingizwa jeshini kupigana vita pia imeongezeka mara tano, huku mshambulizi katika mashule na hospitali yakiongezeka mara mbili.

Wameongeza kuwa kuingiliwa kwa shughuli za kufikisha misaada ya huduma muhimu kwa wahitaji kumewanyima maelfu ya watoto haki zao za msingi za elimu na afya.