Skip to main content

Mwakilishi wa UM nchini Yemen akaribisha usitishaji uhasama:

Mwakilishi wa UM nchini Yemen akaribisha usitishaji uhasama:

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu Umoja wa mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed amekaribisha kuanza usiku wa April 10 kuamkia leo usitishaji uhasama. John Kibego na taarifa kamili..

(TAARIFA YA KIBEGO)

Bwana Ahmed amezitaka pande zote kushirikiana kuhakikisha kwamba usitishaji huo wa mapigano unaheshimiwa na kujenga mazingira muafaka kwa ajili ya mazungumzo ya amani yaliyopangwa kuanza Kuwait mnamo tarehe 18 April.

Amesema pande zote zimehakikisha nia ya kuambatana na matakwa ya usitishaji uhasama yaliyowasilishwa.

Pia amezitaka pande zote na jumuiya ya kimataifa kuunga mkono usitishaji uhasama huo kama ni hatua ya kwanza ya kurejea kwa amani Yemen.

Ameongeza kuwa usitishaji huo ni muhimu, na uliohitajika haraka, kwani Yemen haiwezi kumudu kupoteza maisha ya watu zaidi.