Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na WFP wasaidia wahanga wa ukame Somaliland na Puntland:

UNICEF na WFP wasaidia wahanga wa ukame Somaliland na Puntland:

Huko Kaskazini mwa Somalia shirika la kuhudumia watoto UNICEf na lile la mpango wa chakula duniani WFP wanaongeza juhudi za kuzisaidia jamii kukabiliana na ukame mkali uliochangiwa na El Niño katika majimbo ya Somaliland na  Puntland. Assumpta Massoi anaarifu..

(TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI)

Mashiorika hayo mawili ynashirikliana kukabiliana na hali ya uhaba wa chakula inayoongezeka na kusababisha utapia mlo katika maeneo yaliyoathirika, kwa kuwapa msaada wa kuokoa maisha unaojumuisha chakula, mkakati wa lishe na huduma za afya, pia kuzisaidia jamii kupata fursa ya maji na kuboresha hali ya usafi.

Wakati huu ambapo watoto wengi wanaacha shule na maelfu kukimbia, mashirika hayo yanajikita pia katika kuhakikisha watoto wanasalia mashuleni na kuwalinda wasitengane na familia zao, pia kuwalinda dhidi ya ghasia na unyanyasaji.

Umoja wa mataifa umeomba dola milioni 105 ili kutoa msaada kwa watu milioni 1.7 wengi wakiwa wakulima na wafugaji. Watu 385, 000 kati yao wanahitaji msaada wa haraka.