Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nuru yafikia wakazi wa Deir Ezzor- WFP

Nuru yafikia wakazi wa Deir Ezzor- WFP

Hatimaye misaada muhimu ya kibinadamu imefikia wakazi wa mji wa Deir Ezzor nchini Syria, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwezi Machi mwaka 2014.

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limefikisha msaada huo wa tani 20 ikiwemo maharagwe na mchele vikilenga kutosheleza wakazi 2,500 kwa mwezi mmoja.

WFP imesema misaada hiyo imewasilishwa kwa ndege ya kukodi kutoka Amman, Jordan na iliangushwa kutoka angani kwa wakazi wa mji huo ambao umekuwa umezingirwa kwa takribani miaka miwili sasa.

Kwa sasa WFP inashirikiana na wadau mjini humo kuratibu usambazaji wa misaada hiyo, mingine zaidi ikitarajiwa siku za usoni.