Hali ya kibinadamu Fallujah ni mbaya: UM

9 Aprili 2016

Umoja wa Mataifa umesema umepokea taarifa za kuzorota kwa hali ya kibinadamu katika mji wa Fallujah nchini Iraq.

Taarifa ya ofisi ya mwakilishi mkazi na mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini humo imesema kuwa kutokana na Fallujah kuwa chini ya himaya ya kundi linalotaka dola ya kiisilamu ISIL na washirika wake kumezidisha mateso kwa wananchi wasio na hatia.

Mteso hayo yanachagizwa na kuzingirwa kwa eneo hilo na kushindwa kufikishwa misaada imesema taarifa hiyo.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa kuna taarifa za uhakika kuwa watu wanataka kuondoka eneo hilo kwa ajili ya usalama wao  lakini hawawezi hatua inayotia hofu kuhusu hatma ya Fallujah.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter