Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika iwezeshwe kukabiliana na majanga : O'Brien

Afrika iwezeshwe kukabiliana na majanga : O'Brien

Mkutano kuhusu uwezo wa Afrika katika kukabiliana na majanga ya kibinadamu umefanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo viongozi kadhaa wamehutubia akiwamo Mratibu Mkuu wa masuala ya kibinadamu, Stephen O'Brien ambaye amesema bara hilo linakabiliwa na changamoto zinazohitaji misaada ya haraka.

Mkutano huo umejadili umuhimu wa udharura wa kuchukua hatua, O'Brien aliyewakilisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema bara la Afriak limeathirika pakubwa kupitia majanga.

( SAUTI O’BRIEN)

‘‘Kwa hakika ninasikitishwa na changamoto ambazo mnakabiliana nazo, mthalani madhara ya El-nino na mabaidiliko ya tabia nchi. Inatatiza maisha ya wengi barani. Inaleta hofu kila siku namna watakavyopata chakula na familia zao. Ukame sugu na majanga mengine ya asili yanateketeza sio tu ustawi lakini pia maisha kwa kwaujumla ya mamilioni ya watu.’’

Misaada zaidi ya kifedha kwa wakati inahitajika mtahalani katika kukabiliana na El nino ambapo amesema ni asilimia 20 tu ya fedha zinazohitajika kwa ajili ya kukabiliana na madhara ya janga hilo kimetolewa.

Mratibu huyo Mkuu wa masuala ya kibinadamu amesema wito wa changizo la fedha hivi karibuni kwa Somali, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokraisa ya Congo DRC, Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, na Chad umetimizwa kwa asilimia saba pekee.