OHRC yapinga hukumu ya kifo Bangladesh
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu OHCHR imeelezea kusikitishwa kutokana na hukumu ya kifo dhidi ya watu wawili nchini Bangladesh iliyotolewa na mahakama ya kimatiafa ya uhalifu nchini humo, kwa kuzingatia mchakato wa kimataifa wa haki katika kuendesha kesi.
Katika taarifa yake OHCHR imesema kuwa tangu mwaka 2010 mahakama hiyo imetoa hukumu takribani 17 nyingi kati ya hizo zikiwa za kifo na hadi sasa wanaume wanne wamenyongwa.
Katika hukumu hiyo dhidi ya viongozi wa upinzani Motiur Rahman Nizami na Mir Quasem Ali wa chama cha kiislamu cha Jamaat , Nizam amekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo ya kifo.
Umoja wa Matifa unapinga hukumu ya kifo katika mazingira yoyote yale bila kujali kiwango cha uhalifu na hata kama haki ya hukumu na viwango vimezingatiwa.