Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba kuhusu usalama wa nyuklia kuanza kutekelezwa Mei 2016

Mkataba kuhusu usalama wa nyuklia kuanza kutekelezwa Mei 2016

Mkataba muhimu kuhusu usalama wa nishati ya nyuklia utaanza kutekelezwa mnamo tarehe 8 Mei, ukilenga kupunguza hatari ya kufanyika shambulizi la kigaidi dhidi ya mtambo wa nishati ya nyuklia, na kufanya usafirishaji haramu wa nyenzo za nyuklia kuwa mgumu zaidi.

Hii ni kufuatia idadi inayohitajika ya nchi wanachama zilizoridhia marekebisho ya mkataba huo kutimu 102, baada ya taifa la Nicaragua kuwasilisha hati yake ya kuuridhia hii leo.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA Yukiya Amano anasema leo ni siku muhimu kwa kuwa ..

(Sauti ya Amano)

“Kuanza kutumika kwa marekebisho ya mkataba huu, ni ishara ya azma ya jumuiya ya kimataifa ya kushirikiana kuimarisha usalama wa nyuklia duniani.”

Marekebisho ya mkataba huo yaliyopitishwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, yatalazimu serikali kuwajibika kulinda mitambo ya nyuklia.