Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola bilioni 16 kusaidia mabadiliko ya tabianchi kila mwaka

Dola bilioni 16 kusaidia mabadiliko ya tabianchi kila mwaka

Benki ya dunia imesema kuanza sasa itaelekeza kila mwaka dola bilioni 16 kwa ajili ya miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

(Taarifa ya Grace)

Uamuzi huo umo kwenye sera iliyotangazwa na benki hiyo ikiwa ni hatua ya kimsingi ya mabadiliko ya kisera ambapo sasa itatumia asilimia 28 ya bajeti yake kwenye miradi ya tabianchi ikiwemo nishati endelevu, miji salama na kupunguza hewa chafuzi.

Rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim amesema hatua uamuzi huo wa aina yake unafuatia mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi uliotiwa saini mwezi Disemba mwaka jana na kinachofanyika sasa ni kupitisha uamuzi wa kijasiri ili kulinda sayari na vizazi vijavyo.

Halikadhalika amesema miradi yote ya uwekezaji kuanzia sasa itazingatia suala la kudhibiti mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la joto duniani.