Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano kuhusu kuzuia itikadi kali katili waanza Geneva

Kongamano kuhusu kuzuia itikadi kali katili waanza Geneva

Kongamano la siku mbili kuhusu kuzuia itikadi kali katili limeanza leo jijini Geneva Uswisi, likiwa limeandaliwa na serikali ya Uswisi na Umoja wa Mataifa.

Kongamano hilo ambalo limetokana na mpango wa Katibu Mkuu wa kuchukua hatua za kuzuia itikadi kali katili na mjadala wa Baraza Kuu wa Februari 12 na 16, 2016, litatoa fursa kwa jamii ya kimataifa kubadilishana mawazo kuhusu uzoefu na mbinu bora za kukabiliana na vyanzo vya itikadi kali katili.

Aidha, kongamano hilo litatumiwa kuimarisha uungaji mkono kwa mpango wa Katibu Mkuu wa kuchukua hatua.

Akihutubia uzinduzi wa kongamano hilo, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Michael Moller, ameeleza jinsi itikadi hiyo inaathirika raia wa dunia nzima.

(Sauti ya Bwana Moller)

Itikadi kali na katili imebadilisha ainaa ya mizozo. Kupitia vitendo vyao, kwa kutawala maeneo, kudharau mipaka ya kimataifa, kukiuka haki za binadamu na kutumia Intanet na mitandao ya kijamii kushawishi uhalifu wao, vikundi kali na katili wanajaribu kuathiri maadili yetu ya pamoja ya amani, haki na utu.”

Naye Martin Kimani ambaye ni mkurugenzi wa kitengo cha kukabiliana na ugaidi cha kitaifa Kenya, nchi ambayo imeshuhudia ugaidi ..

"Nchini Kenya tunaamini umuhimu wa mikakati inayoongozwa kitaifa na kwa sababau hiyo tunaamini kwamba majadiliano ni muhimu na kuweka mikakati ya kukabiliana na itikadi kali inayoendana na uhalisia wa kitaifa na mashinani, kwa ulelewa kwamba taifa licha ya kwamba mikakati hii lazima ijumuishe mashirika ya kiraia lakini serikali hazipaswi kuenguliwa.”