Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzalishaji wa nafaka duniani watabiriwa kuwa mzuri 2016, ingawa chini kidogo

Uzalishaji wa nafaka duniani watabiriwa kuwa mzuri 2016, ingawa chini kidogo

Uzalishaji wa nafaka duniani mwaka huu wa 2016 unatarajiwa kufikia tani milioni 521, ikiwa ni upungufu wa asilimia 0.2 tu kutoka kwa uzalishaji mkubwa wa mwaka jana.

Kwa mujibu wa utabiri wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) kwa msimu huu mpya, kiwango cha uzalishaji cha mwaka huu kitakuwa cha tatu kwa ukubwa katika rekodi za kimataifa.

FAO imesema, kiasi kikubwa cha akiba ya chakula na kiwango kidogo cha ununuzi kimataifa vinamaanisha kuwa soko la nafaka za chakula kinachotegemewa halitabadilika sana kwa angaa msimu mmoja.

Wakati huo huo, FAO imetoa takwimu za kiwango wastani cha bei ya chakula mnamo mwezi Machi, zikionyesha kuwa kwa ujumla, bei ilipanda kwa asilimia 1.0 mwezi Machi ikilinganishwa na Februari, ambapo kupanda kwa bei ya sukari na mawese kulisaidia kuokoa uzani kwa upande wa bidhaa za mifugo ambazo bei yake imeendelea kushuka.