Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utajiri wa Afrika unufaishe wote ili kuondokana na njaa- FAO

Utajiri wa Afrika unufaishe wote ili kuondokana na njaa- FAO

Bara la Afrika limepiga hatua kubwa katika kukabiliana na njaa kati mwaka 1990 hadi 2015 lakini mabadiliko ya tabianchi, mizozo na ukosefu wa usawa wa kijamii vinaendelea kutia giza harakati za bara hilo kujikwamua dhidi ya njaa na uhakika wa chakula. Taarifa kamili na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Ni kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO Jose Graziano da Silva aliyotoa huko Abidjan Cote d’Ivoire kwenye mkutano wa shirika hilo kanda ya Afrika.

Amesema ingawa kiwango cha watu wenye njaa barani humo kimepungua kwa asilimia 30 katika kipindi hicho, bado uhaba wa chakula unashuhudiwa katika baadhi ya maeneo, ukuaji wa uchumi ukinufaisha wachache.

Ametaka nchi za Afrika kuzingatia maudhui ya mkutano huo ya kubadili mifumo ya kilimo na chakula Afrika kwa maslahi na ustawi wa wote wakati huu ambapo baadhi ya nchi zinashuhudia maliasili zikitumiwa kupindukia kwa manufaa ya wachache, wakazi wa vijijini wakisalia hohehahe.