Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumechukua hatua dhidi ya askari walinda amani: Tanzania

Tumechukua hatua dhidi ya askari walinda amani: Tanzania

"Tumechukua hatua kadhaa, taifa limedhalilishwa'' ni sehemu ya maneno ya mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini New York balozi Tuvako Manongi akizungumzia tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazowakabili walinda amani 11wa nchi hiyo walioko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami, balozi Manongi amesema kuwa amearifiwa na wizara ya mambo ya nje kuhusu namna tuhuma hizo zilivyokera taifa na akasema vitendo hivyo havitafumbiwa macho.

Bila kuuma maneno Balozi Manongi anaanza kwa kusema hatua stahiki zilizochukuliwa.