Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya kuwa na mtambo wa nishati ya jua mkubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati

Kenya kuwa na mtambo wa nishati ya jua mkubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati

Katika kutekeleza miradi ya nishati endelevu isiyoharibu mazingira, Kenya imeidhinisha mradi wa nishati ya jua utakaogharimu dola Milioni 126 na kwa ajili ya kukwamua kaya zaidi ya Laki Sita.

Tovuti ya Climate Action inayoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP katika kusaka miradi ya nishati endelevu kwa mazingira, imesema mtambo huo utakaojengwa Garissa, mashariki mwa Kenya kwa usaidizi wa China, utazalisha Megawati 55.

Kwa mujibu wa mamlaka ya usambazaji umeme vijijini Kenya, REA mtambo huo wa nishati ya jua utakuwa mkubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na ujenzi unatarajiwa kuanza mwezi Julai.

Umeme kutokana na mradi huo utakaotoa ajira zaidi ya Elfu Moja unatarajiwa kuunganishwa kwenye gridi ya taifa ndani ya mwaka mmoja.