Skip to main content

Michezo ni nyenzo muhimu katika kuchagiza utu na haki:Ban

Michezo ni nyenzo muhimu katika kuchagiza utu na haki:Ban

Michezo ni njia ya kipekee na muhimu katika kuchagiza utu na usawa na haki ya kila binabamu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wake maalumu kwa siku ya kimataifa ya michezo kwa ajili ya maendeleo na amani.

Ameongeza kuwa pia ni hamasa ya kuleta mabadiliko ya kijamii, na ndio maana wanamichezo nyota wamesalia katika kujihusisha na kuusaidia Umoja wa mataifa kuelimisha kuhusu masuala muhimu kama njaa, HIV na ukimwi, usawa wa kijinsia na kulinda mazingira.

Amesema mwaka huu dunia inajikita katika kuanza kwa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu kwa minajili ya ajenda ya 2030 na ili kufikia malengo, amesema ni lazima kuhusisha sekta zote za jamii kila mahali.

Katika siku hii ametoa wito kwa serikali, mashirika, makampuni ya biashara na wadau wote katika jamii kuenzi thamani na uwezo wa michezo katika kufikia malengo hayo 2030. Naye mshauri maalumu wa masuala ya michezo kwa ajili ya maendeleo na amani Wilfred Lemke akiunga mkono umuhimu wa michezo katika ajenda ya 2030 amesema.

(SAUTI WILFRED LEMKE)

“Umoja wa Mataifa unawakaribisha nyote kushiriki kampeni yetu”tucheze kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu, kuchagiza siku hiyo pamoja na mchango wa michezo kwa SDG’s. Siku hii ni fursa ya jumuiya ya kimataifa kuja pamoja kushereheka na kushirikiana.Michezo ni kwa wote na kila mmoja ni lazima ashiriki.”