Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani machafuko Brazzaville

UM walaani machafuko Brazzaville

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kwa Afrika ya Kati, Abdoulaye Bathily amelaani machafuko yaliyotokea kwenye maeneo ya Brazzaville, nchini Jamhuri ya Congo siku chache zilizopita na kusababisha raia kukimbia makwao.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika ya Kati, Bwana Bathily ameeleza kufuatilia kwa karibu hali iliyopo sasa nchini humo, wiki mbili tu baada ya kuchaguliwa upya kwa rais Denis Sassou-Nguesso.

Amezisihi pande zote, hasa wadau wa kisiasa na vikosi vya usalama, kuwajibika na kujizuia na vitendo vyovyote vitakavyohatarisha utulivu wa nchi.

Amesisitiza kwamba mazungumzo na upatanisho ndio suluhu kwa mivutano inayoweza kuibuka baada ya uchaguzi.