Ulaya inakaribia kutokomeza surua na rubella:WHO
Nchi 32 barani Ulaya zimefanikiwa kudhibiti maambukizi ya maradhi ya surua na rubella kwa mujibu wa hitimisho la uhakiki wa kamisheni ya Ulaya ya kutokomeza surua na rubella uliotolewa leo.
Dr Zsuzsanna Jakab mkurugenzi wa kanda ya Ulaya wa shirika la afya duniani WHO amesema kudhibiti maambukizi ya maradhi hayo kwa zaidi ya nchi za Ulaya kunadhihirisha kwamba kutokomeza Surua na rubella katika kanda hiyo kunawezekana kwa kwamba wako katika njia sahihi ya kufikia lengo hilo.
Ameongeza kuwa kasi lazima iendelee ili kuendelea kuhakikisha mafanikio hayo ambako kunayumba na kuhakikisha nchi ambazo bado hazijafanikiwa zinajitahidi haraka kufanya hivyo.
Tathimini imefanyika kwa nchi wanachama ili kuangalia hatua iliyopigwa katika kutokomeza surua na rubella kwa kuangalia takwimu za maabara zilizowasilishwa nan a kamati ya kila nchi ambazo sasa zipo katika nchi 50 kati ya 53 za Ulaya.
WHO imesema itaendelea kuzisaidia nchi hizo kwa msaada wa kiufundi na ushauri hadi pale lengo la kutokomeza surua na rubella litakapofikiwa.