Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwepo wa mabomu ya ardhini bado ni tishio kubwa kwa maisha ya watu Afghanistan:UNAMA

Uwepo wa mabomu ya ardhini bado ni tishio kubwa kwa maisha ya watu Afghanistan:UNAMA

Kuwepo kwa mabomu na vifaa vingine vya mlipuko nchini Afghanistan bado ni tishio kubwa kwa maisha na vipato vya maelfu ya raia wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa ripoti ya mpango wa Umoja wa mataifa nchini Afghanistan UNAMA, wakati wa mwaka 2015, Waafghanistan 388 waliuawa au kujeruhiwa kwa mabomu na vifaa vya mlipuko.

Aidha, vifaa vya milipuko vilikuwa hatari kubwa, na kusababisha majeruhi kwa raia 1,051 ikiwa ni pamoja na vifo 459 mwaka 2015.

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya uelewa wa mabomu na msaada katika hatua dhidi ya mabomu Rafiullah Alkozai kutoka UNAMA amezungumza na Mheshimiwa Mohammad Wakil afisa katika mpango wa Umoja wa mataifa wa hatua dhidi ya mabomu nchini Afghanistan

(SAUTI YA MOHAMMAD WAKIL)

Mpango wa hatua dhidi ya mabomu Afghanistan unatoa elimu kwa watu milioni 20 raia wa Afghanistan, na tumefanikiwa kwa ushirikiano na wizara ya elimu kutoa elimu mashuleni na kuingiza kwenye mtaala wa shule elimu hiyo kwa wanafunzi wa darasa la 3 hadi la 12. Mwaka jana tulitoa mafunzo kwa maimamu zaidi ya 10,000 ili wafikishe elimu ya hatua dhidi ya mabomu misikitini katika salaa ya Ijumaa.”