Skip to main content

Kamisheni ya Kuondoa Silaha yaanza kikao chake cha 2016

Kamisheni ya Kuondoa Silaha yaanza kikao chake cha 2016

Kamisheni ya kuondoa silaha imeanza kikao chake cha mwaka 2016 leo jijini New York, ambapo Mwakilishi wa ngazi ya juu kuhusu masuala ya uondoaji silaha, Kim Won-soo, amesema Kamisheni hiyo inaanza kikao hicho wakati wa migawanyo mikubwa kuhusu suala la uondoaji silaha, zikiwemo za nyuklia. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Bwana Won-soo amesema kushindwa kuanza kutekeleza mkataba wa kina wa kupinga majaribio ya silaha za nyuklia, pamoja na kutokuwepo mashauriano zaidi kuhusu suala hilo miongoni mwa nchi wanachama ni mambo yanayovunja moyo.

Kwa mantiki hiyo, Bwana Won-soo amesema wengi wamelazimika kutafuta njia mpya nje ya mfumo wa Umoja wa Mataifa, ili kuendeleza kazi ya kupiga hatua. Hata hivyo, ameelezea matumaini yake kuhusu Kamisheni hiyo

“Kamisheni hii ina uwezo mkubwa wa kudhihirisha kuwa mfumo uliopo wa kuondoa silaha unaweza kuzaa matunda. Hivi karibuni, Kamisheni imepiga hatua muhimu kuelekea muafaka kuhusu suala la silaha zinazokubalika. Hii ni kufuatia hatua muhimu zilizopigwa na jamii ya kimataifa kuhusu sehemu hii ya uondoaji silaha”