Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila vita kukomeshwa mabomu ya ardhini yatasalia tishio: Owusu

Bila vita kukomeshwa mabomu ya ardhini yatasalia tishio: Owusu

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuelimisha kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na vifaa vya milipuko, Sudan Kusini moja ya nchi zilizoathiriwa na vita nayo pia imeangazia siku hiyo kwenye mji mkuu Juba.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini humo Eugen Owusu amesema kwa ushirikiano na wadau ikiwemo mamlaka ya kitaifa ya kudhibiti mabomu wameweza kuelimisha na kuteketeza matenki milioni moja lakini anasema.

( SAUTI OWUSU)

‘Pale machafuko yanapoendelea mazingira mapya yanasalia kuhatarisha umma. Kwa sasa kuna maeneo hatari 871ambayo yamesalia kuondolewa mabomu na mengine zaidi yakiripotiwa kila siku.”

Amesema Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau utasaidia jamii zilizoko hatarini zaidi kuchukua hatua.