Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN-Habitat yaombleza kifo cha Dame Zaha Hadid

UN-Habitat yaombleza kifo cha Dame Zaha Hadid

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa makazi, UN-Habitat, limetoa taarifa ya kuomboleza kifo cha Dame Zaha Hadid, ambaye alikuwa mmoja wa wasanifu majengo mashuhuri zaidi duniani.

Akijulikana kama msanifu majengo aliyejikita katika kuvuka mipaka ya usanifu majengo na miundo ya makazi ya miji, kazi ya Bi Hadid, ilifanyia majaribio dhana mpya za ujenzi kwa ujasiri, na hivyo kuchangia miundo mipya ya mipango ya makazi ya mijini na miundombinu.

Akitoa rambirambi zake kwa familia yake na watu wa taifa la Iraq, Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Habitat, Dkt. Joan Clos amezitaja habari za kifo cha Bi Zaha Hadid mnamo Alhamis Machi 31, 2016 kama za kutia huzuni, kwani alikuwa mfano wa kuwapa hamasa wasanifu majengo wanawake, na aliweza kupenya na kupata ufanisi mkubwa katika fani inayotawaliwa na wanaume.