Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabomu ya ardhini ni changamoto ya kibinadamu:Ban

Mabomu ya ardhini ni changamoto ya kibinadamu:Ban

Kukabiliana na athari za mabomu ya ardhini na vifaa vingine vya mlipuko katika maeneo ya vita ni changamoto kubwa ya kibinadamu amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon. Taarifa ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi.

(TAARIFA YA GRACE)

Katika ujumbe wake maalumu kwa ajili ya siku ya kimataifa ya kuelimisha kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini , Ban ameelezea hofu yake hususani kuhusu matumizi ya silaha za mlipuko katika maeneo yenye kadamnasi.

Amesema Umoja wa mataifa unachukua hatua kusaidia jamii zilizoathirika ambazo ziko katika hatari kubwa ya kimazingira zikiwemo Sudan Kusini na Syria ambapo lengo ni kuwa na amani ya kudumu.

Ameongeza kuwa raia na watu wasio wapiganaji ndio waathirika wakubwa wa mabomu ya ardhini na mabomu mtawanyiko, akitia msisitizo katika kuali mbiu kwamba “hatua dhidi ya mabomu ni hatua ya kibindamu."

Bruno Donat ni msemaji kutoka ofisi ya Umoja wa Mataiaf inayohusika na kampeni dhidi ya mabomu hayo, UNMAS

(SAUTI YA BRUNO)

 “Mabomu ya ardhini yanaua takribani watu 10 kila siku duniani kote na kujeruhi vibaya wengine wengi, na asilimia 40 ya majeruhi hao ni watoto”