Umuhimu wa misitu nchini Uganda

1 Aprili 2016

Misitu ni uhai!

Misitu huleta maji, chakula, hewa safi, mazingira bora na mambo kadha wa kadha!

Jumuiya ya kimataifa kwa kutambua umuhimu wa rasilimali hii ilipitisha tarehe ishirini na moja mwezi Machi kila mwaka kuwa  maadhimisho ya siku ya Misitu Duniani. Maadhimisho ya mwaka huu yaliangazia umuhimu wa misitu kama chanzo cha asilimia thelathini ya maji ya aslili ambayo hutumiwa viwandani na majumbani.

Katika ujumbe wake wa siku hiyo mwaka huu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipigia chepuo, kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kutetea rasilimali hiyo adhimu.

Nalo shirika la Chakula na Kilimo, FAO katika kuenzi siku hii limezindua mpango mpya kwa lengo la kuongeza fursa ya umuhimu wa misitu katika kuboresha hadhi ya maji na upatikanaji wake.

Mpango huu utajikita zaidi katika uhusiano baina ya misitu na maji na utaanza kwa kuangalia njia za kuboresha usalama wa maji katika nchi nane za Afrika ya Magharibi ambazo ni Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Mali, Mauritania, Niger, Senegal na Sierra-Leone

Tukisalia barani Afrika hususani Mashariki mwa bara hilo nchini Uganda, John Kibego anatupeleka mgharibi mwa taifa hilo kumulika hatima ya bwawa la umeme la Kabalega linalotegemea maji ya Mto Wambabya, ambao kwa sasa unachafuliwa kwa kiasi kikubwa.

(KIBEGO PACKAGE)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter