Skip to main content

Watu zaidi ya 1000 wameuawa Iraq kwa mwezi Machi pekee:UNAMI

Watu zaidi ya 1000 wameuawa Iraq kwa mwezi Machi pekee:UNAMI

Jumla ya watu 1119 raia wa Iraq wameuawa na wengine zaidi ya 1500 kujeruhiwa katika matukio ya kigaidi, machafuko na vita nchini Iraq katika mwezi wa Machi mwaka huu kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mpango wa Umoja wa mataifa wa msaada kwa Iraq UNAMI.

Takwimu hizo zinasema idadi ya raia waliokufa ni 575, wakiwemo polisi 45 huku waliojeruhiwa ni 1,196 wakijumuisha polisi 50.

Imeongeza kuwa upande wa vikosi vya ulinzi na usalama askari 544 wa majeshi ya Iraq wakiwemo wa Peshmega, SWAT na wanamgambo wanaopigana sambamba na jeshi la Iraq waliuawa huku wengine 365 wakijeruhiwa kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Iraq bwana Mr. Ján Kubiš, , kwa ujumla idadi ya vifo imeongezeka ikilinganishwa na miezi iliyopita, na amesema anahofia hali ya kuendelea kwa machafuko na kupotea kwa maisha ya watu pia kujeruhiwa nchini humo.