Japan imetoa dola milioni 4 kwa IOM kusaidia wakimbizi wa ndani Iraq na wasyria

1 Aprili 2016

Serikali ya Japan inatoa dola milioni 4 kwa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM Iraq ili kusaidia wakimbizi wa ndani Iraq na wakimbizi wa Syria .

Mchango huu utalisaidia shirika la IOM kukabiliana na hali ya sasa ya kibinadamu na mtafaruku wa wakimbizi wa ndani nchini Iraq, na pia  ufadhili miradi miwili katika kipindi cha miezi 12.

Dola milioni 3.2 kati ya hizo zitatumika kusaidia wakimbizi wa ndani kupitia mradi wa IOM ujulikanao kama “mpango wa dharura na ufufuaji wa jamii kwa ajili ya wakimbizi wa ndani, wanaorejea na jamii zinazowahifadhi nchini kote Iraq.” Mradi huo itajikita katika kujenga malazi la muda kwa kutumia vifaa vinavyopatikana hapo hapo Iraq.

Dola zingine 500,000 zitatumika kuwasaidia wakimbizi wa Syria na jamii zinazowahifadhi zilizoko Iraq kupiotia mradi mwingine wa IOM, ambao ni “mpango wa dharura na msaada kwa wakimbizi wa Syria nchini Iraq”.

Miradi hii inaenda sanjari na mkakati wa IOM wa kutoa msaada kwa makundi ya watu wasiojiweza nchini Iraq kwa ushirikiano na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter