Vifo vya raia vyaendelea kuripotiwa Libya

Vifo vya raia vyaendelea kuripotiwa Libya

Nchini Libya, raia 21 wameuwa mwezi Machi, wakiwemo watoto saba, umesema leo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSMIL.

Kwenye taarifa yake, UNSMIL imeongeza kwamba watu wengine 11 wamejeruhiwa, na kwamba Tunisia imeripoti pia wahanga kadhaa kutokana na machafuko nchini Libya. Sababu ya vifo na majeraha haya ni silaha, makombora na mabomu.

Aidha UNSMIL imeeleza kwamba wanaume 18 waliodaiwa kuwa waasi wa vikundi vya kigaidi wameuawa na askari wa vikundi viliyojihami.