Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchini CAR, bado juhudi zahitajika kupambana na ubakaji: Samantha Power

Nchini CAR, bado juhudi zahitajika kupambana na ubakaji: Samantha Power

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kushtushwa sana na ripoti mpya za ukatili wa kingono unaodaiwa kufanywa na walinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Amesema Umoja wa Mataifa utafanya bidii zote ili kupambana na janga hili, akizisihi nchi husika kuchukua hatua thabiti sambamba na zile za Umoja wa Mataifa.

Kauli hiyo pia imetotolewa na Mwakilishi wa Kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Samantha Power ambaye alikuwa ziarani nchini CAR pamoja na mkuu wa idara ya ulinzi wa aman iwa Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous.

Baada ya kukutana na familia za wasichana waliobakwa, Bi Power amekaribisha hatua zilizochukuliwa tayari na uongozi wa Ujumbe wa Umoja wa MAtaifa nchini humo MINUSCA, akisema jitihada zaidi zinahitajika

(Sauti ya Bi Power)

"Askari hao walioshtakiwa kubaka hawajawajibishwa. Kwa hiyo ukiwa askari, unaamini kwamba utakwepa sheria, kwa sababu hakuna uwajibikaji bado. Kwa hiyo uongozi unajua hivyo na unajaribu kuvikabili, lakini lazima kazi kubwa ifanyike kwenye miji mikuu ya nchi hizo zinazotuma askari nchini CAR."