Skip to main content

Wahamiaji takribani 170,000 wameingia Ulaya kupitia Mediterranean:IOM

Wahamiaji takribani 170,000 wameingia Ulaya kupitia Mediterranean:IOM

Takribani wahamiaji na wakimbizi 170,000 wameingia Ulaya kupitia bahari ya Mediterranean katika miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka huu kwa mujibu wa takwimu za shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Takwimu hizi zinatokana na kuwasili kwa karibuni kwa wakimbizi na wahamiaji zilizoripotiwa Alhamisi Italia, lakini pia maelfu wanaoaminika kuingia Ulaya kupitia Hispania.

Idadi hiyo ni karibu mara nane zaidi ya wakati kama huo mwaka 2015. Pia watu zaidi ya 600 wamearifiwa kufa maji katika safari hizo.