Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lajadili UNMISS

Baraza la Usalama lajadili UNMISS

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limejadili hali ya Sudan Kusini. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA HASSAN)

Akizungumza kwenye kikao hicho mwenyekiti wa tume ya pamoja ya ungalizi natathimini bwana Festus Mugae amesema masuala ya utekelezaji wa mkataba wa amani nchini Sudan kusini bado yanakwenda polepole na mchakato wa kuwa na serikali ya mpito unaendelea.

Hata hivyo amesema pande zote zimethibitisha nia ya kutekeleza mkataba huo ikiwa na ana Imani kwamba serikali ya mpito itakuwa madarakani hivi karibuni.

(SAUTI YA FESTUS MUGAE)

Ingawa hili limechelewa kwa miezi kadhaa, ni hatua muhimu kwenda mbele, katika kutekeleza makubaliano, ambayo nimekaribisha. Pande husika zinaweza kufanya juhudi zaidi kujiandaa kwa kurejea kwa makamu wa rais wa kwanza mteule anarudi Juba, na kuhakikisha kuwa kuundwa kwa serikali mpya hakuleti vurugu.”

Amesema kuna muda mchache saana wa kupoteza katika kuhakikisha mkataba wa amani unatekelezwa.

Naye mwakilishi wa katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Sudan Kusini UNMISS na mkuu wa mpango huo Ellen Margaret Loj amesema machafuko bado yanaendelea Sudan licha ya juhudi..

(SAUTI YA LOJ)

"licha ya kusaini mkataba wa makubaliano ya amani, vurugu bado zinaendelea katika maeneo mengi nchini. Katika jimbo la Upper Nile, mvutano kati ya Dinka na Wawshuluk, bado ni wa hali ya juu, kufuatia kuzuka kwa vurugu katika kituo cha ulinzi wa raia cha Malakal hapo februari."